SMASSE Cascade System 5. Kujisimamia/tosheleza kwa hali na mali

Kuhusu swala la kujitosheleza, mradi wa SMASSE uko na aina tatu za kuangalia:-
1. hazina 2. utaalam 3. uongozi;
na uhusiano wake unaonyeshwa na pembe tatu hapa chini

5-1 Hazina
Mradi wa SMASSE unadhaminiwa na serikali za Kenya na Japan, kupitia JICA.

GOK (Government of Kenya, Serikali ya Kenya ):
Serikali ya Kenya husimamia asilimia 40%; 18% hutoka moja kwa moja serikalini na 22% hutoka kwa Halimashauri za Elimu Wilayani, zitokazo kwa lile fungu la ujenzi..

Pesa kutoka kwa halimashauri za elimu wilayani zitaendelea kupatikana kwa sababu:-
(1) shule zitaendelea kutoza karo
(2) shule zahitajika kutoa kati ya asilimia 5% hadi 10% ya pesa hii ya ujenzi (kulingana na mapendekezo ya wilaya).

Pesa zitokazo moja kwa moja serikalini hugharamia matumizi ya mradi ya kila siku, kulipa mishahara ya walimu wa Kenya, na kugharamia vyumba na vifaa vyengine.

Pesa zitokazo wilayani hutumika kwa vyakula, malazi, kulipa walimu wanaotoa mafundisho na kugharamia kusafiri kwa walimu.

Pia hununua na kurebisha vifaa vyengine vihusuvyo utekelezaji wa washa.

JICA:
hutoa pesa za kununua vifaa vya kufundishia walimu kwa kiwango cha kitaifa na hata cha wilayani.

Vifaa hivyo ni pamoja na komputa, projekta, video kamera, TV pamoja na madawa yatumikayo mahabrani, na mengineyo mengi. Vifaa hivi huwekwa katika vituo wakilishi wiliyani.

Pesa za JICA pia husimamia gharama ya walimu wa Kenya waendapo kusomea ujuzi zaidi huko Japan na kulipa mishahara ya walimu wanaotoka Japan kufanya kazi na mradi huu.

5-2 Utaalam
Wafanyakazi:
Serikali ya Kenya imetoa walimu wafanye kazi kwa mradi huu, huku Japan ikitoa walimu wake ili waje wasaidiane; kuanzia mashinani(mipango) hadi utekelezaji.

Walimu kwa pamoja hutayarisha vifaa vya kufundishia kwa kiwango cha kitaifa. Walimu wa wilayani wanahitajika kujibadilishia vifaa hivi kulingana na mahitaji na mazingira yao.

Ijapo walimu wa Japan watarudi kwao baada ya wakati wa mradi kumalizika, wale wa Kenya wataendelea kuwafundisha walimu wengine.

Hata wale wanaofundisha kwa kima cha wilaya pia wataendelea kufanya vivyo hivyo kwani daima kutakuwa na maswala ya kikazi yatakayohitaji washa.

5-3 Uongozi
Muundo wa uongozi:
Mradi huu ni mali ya idara ya Ukaguzi, katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi. Daraja za uongozi wa mradi huu ni kama ifuatavyo:-

Policy:
Msimamo wa serikali ni kuwa ifikapo mwaka wa 2020, uchumi wake utahusisha viwanda, na njia moja ya kufanya hivyo ni serikali kutenga mahali walimu wanaweza kuenda na kukuza ujuzi wao.


Juu