3. Madhumuni ya washa na ASEI/PDSI
Kila washa huwa na lengo. Kwa kila mwaka madhumuni ya washa ni kama inavyoonyeshwa hapa chini:-
Ili kuhakikisha masomo mema kwa hesabu na sayansi na kutarajia mabadiliko kabambe, mradi umetilia maanani mwenendo wa ASEI;
tafsiri yake ikiwa ni Vitendo wakati wa masomo, Wanafunzi, Majaribio ya kimahabra na Mwigizo wa vifaa vikosekanavyo.
ASEI ni neno maarufu ambalo huboresha ufundishi na kumleta mwanafunzi katikati ya masomo, sio mwalimu.
Utaratibu huu humpa mwanafunzi fursa ya kujifanyia kazi za kuhusiana na mahabra ambazo humuwezesha kuelewa na kufahamu masomo ya hesabu na sayansi.
Pia ikumbukwe kuwa, vifaa halisi vikosekanapo, mwalimu anapaswa kutumia vile vya asili vipatikanavyo katika sehemu hiyo. Hatua hii pia humfanya mwanafunzi avutiwe na masomo.
![]() |
![]() |
![]() |
|
|
Maonyesho
|
Mazungumzo
|
Somo la ASEI
|
Masomo ya ki-ASEI huwezekana kwa utaratibu wa Tayarisha, Tekeleza, Chunguza, Boresha.
Hali hii hufanya masomo kuwa na maana na kumfanya mwanafunzi aelimke na kuwa ujuzi ufao.